Huenda Simba siku ya kesho Jumatatu ikapeleka machungu mengine kwa watani zao Yanga pale watakapotangaza usajili wa kiungo Mcongomani Papy Kabamba Tshishimbi
Pamoja na Yanga kutangaza kuachana na mchezaji huyo, lakini inafahamika walishindwa kumlipa dau la usajili alilotaka kulinganisha na ofa ambao inaelezwa aliwekewa mezani na mabingwa wa nchi, Simba
Mara kwa mara Tshishimbi amehusishwa na klabu ya Simba, na hata yeye mwenyewe mara nyingi ameonyesha kutamani kucheza na nyota wa Simba
Msimu uliomalizika haukuwa mzuri sana kwake kutokana na majeraha aliyokuwa akipata mara kwa mara, alikuwa akifanya kazi kubwa sana pale Yanga
Hakuna shaka, kama atasajiliwa, ndani ya Simba atafanya kazi nzuri zaidi kwani huku timu imekamilika
ADVERTISE HERE