Msimu uliomalizika utaingia kwenye kumbukumbu za klabu ya Simba kuwa moja ya misimu ambayo mabingwa hao wa nchi wamepata mafanikio makubwa
Wababe hao wa soka hapa nchini wametwaa mataji yote ya michuano ya ndani, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na kombe la FA hii ni kwa upande wa timu ya Wanaume
Lakini dada zao nao wa Simba Queens jana wakaongeza taji la nne la ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake wakitwaa taji hilo huku wakiwa na mechi mbili mkononi

Haya ni mafanikio makubwa kwa taasisi ya Simba ambayo yanaakisi matunda ya Uwekezaji Mkubwa uliofanywa na Bilionea Mohammed Dewji 'Mo', Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
Simba ina mkakati kabambe wa kuunda timu imara ya vijana pia ili kuhakikisha wanaendelea kutawala soka la Tanzania katika nyanja zote
Ile ahadi ya kushinda mataji kwa miaka 10 mfululizo bado iko palepale