Tuzo za wachezaji bora msimu wa 2019/20 zinatarajiwa kutolewa siku ya kesho Ijumaa, August 07 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
Miongoni mwa tuzo hizo, ipo tuzokubwa kabis aya mchezaji bora wa msimu ambayo inawaniwa na wachezaji watatu, Clatous Chama, Bakari Mwamnyeto ambaye msimu uliomalizika alikuwa Coastal Union na Nicholas Wadada wa Azam Fc
Chama pia anawania tuzo ya kiungo bora wa msimu
Kwa kuangalia takwimu tu, ni wazi hakuwezi kuwa na mjadala juu ya nani anayestahili tuzo ya kushinda mchezaji bora wa msimu, ni Clatous Chama
Msimu huu ulikuwa bora sana kwa Chama, kwani aliwapa burudani mashabiki, alifunga mabao lakini pia alitoa pasi za mabao
Jumla Chama amefunga mabao sita na pasi 13 akiwa amefunga mabao mawili ndani ya ligi na mabao manne Kombe la Shirikisho, pasi 10 ni Kwenye ligi na tatu ni za Shirikisho
Ndio maana hata msemaji wa Simba Haji Manara amefunguka kuwa Chama ana vigezo vya kubeba kila tuzo na litakuwa jambo la kushangaza kama hatapewa tzuo hizo