Mfungaji bora ligi kuu ya Vodacom misimu ya 2018/19 na 2019/20 Meddie Kagere ataendelea kubaki sana na machampioni wa nchi, Simba baada ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja
Kagere alikuwa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Simba na sasa ataendelea kuwepo Msimbazi mpaka mwaka 2022
Patrick Gakumba ambaye ni wakala wa mchezaji huyo amethibitisha kuwa mabosi wa Simba wameridhishwa na kazi yake hivyo wameamua kumuongeza mwaka mwingine na sasa kuwa na miaka miwili kwenye mkataba wake
Kagere amerejea kwao Rwanda kwa ajili ya mapumziko kama ilivyo kwa wachezaji wote wa Simba ambao wanatarajiwa kurejea wiki ijayo kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ambao utaanza Septemba 06 2020
ADVERTISE HERE