Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema mlinda mlango Beno Kakolanya bado ana mkataba na mabingwa hao wa nchi na hawana mpango wa kumuuza
Kwa siku za karibuni kumekuwa na tetesi zinazomuhusisha Kakolanya na klabu ya Azam Fc ambayo imetangaza kuachana na Mghana Razak Abarola huku wakitaja nafasi yake kutarajiwa kuchukuliwa na kipa mzawa
Senzo amesema Beno ni mchezaji halali wa Simba na hawafikirii kumuuza
"Beno bado anamkataba wa Sisi kwahiyo tutaendelea kuwa nae na hatuwezi kumuuza na wala kumtoa kwa mkopo kwenda kokote," alisema Senzo
Kakolanya amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza mbele ya Tanzania One, Aishi Manula
ADVERTISE HERE