Kwa huyu Miquissone Simba imewekeza kwelikweli

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Aug 2020
Kwa huyu Miquissone Simba imewekeza kwelikweli

Mwanahabari na mchambuzi wa masuala ya soka nchini Shaffih Dauda amezipa ujumbe timu zinazotaka mafanikio, zinapaswa kufanya uwekezaji mkubwa kwa kununua wachezaji wenye hadhi kama kina Luis Miquissone

Shaffih amewaambia kwa aina ya usajili ambao baadhi ya timu wanafanya, wasitarajie kushindana na Simba kwani mabingwa hao wa nchi wanapiga hesabu zao vyema na wanatumia pesa kutengeneza timu imara

"Simba imemsajili Luis Miquissone kutoka Mamelodi Sundowns akiwa kwa mkopo UD Songo. Klabu kama Mamelodi ikikubali kumsajili mchezaji na kumuweka kwenye mifumo yao ujue kuna kitu cha ziada wanakiona," alisema Shaffih

"Umeshawahi kujiuliza Simba ililipa kiasi gani kumpata Miquissone? Simba ililipa ada ya uhamisho inayokaribia Tsh. 700m (USD 300,000) hiyo ni ada ya uhamisho ambayo ililipwa timu. Achana na pesa ambayo amelipwa Miquissone"

"Kwa hiyo Miquissone ameigharimu Simba si chini ya Bilioni! Mkataba wake ni muda mrefu Simba kwa hiyo thamani yake ni zaidi ya Bilioni"

"Miquissone anachokifanya uwanjani si maajabu, ila anafanya kulingana na thamani yake. Nadhani hadi sasa hakuna Mtanzania ambaye ana shaka na uwezo wake"

"Kwa hiyo kama huna mzigo wa kuwekeza kwa ajili ya kusajili wachezaji wa viwango vya juu, utanunua wachezaji wa kawaida hivyo usitegemee kushindania ubingwa"

Miquissone alitua Simba usajili wa dirisha dogo mwezi Januari 2020 akisaini mkataba wa miaka mitatu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’