Baada ya kukamilisha msimu kibabe kwa kutwaa mataji matatu 'treble', uongozi wa klabu ya Simba unatarajiwa kuanza kuweka hadharani majina ya nyota waliosajiliwa pamoja na wale wanaopewa mkono wa kwaheri
Jana Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' alidokeza kuwa hawatarajii kufanya usajili mkubwa sana kwani wana timu imara
Simba inaelezwa kuwa tayari imeshakamilisha usajili wa wachezaji wa ndani
Nyota wa ndani wanaotajwa kumalizana na Simba ni mshambuliaji Charles Ilanfya kutoka klabu ya KMC, mlinzi wa kulia Kameta Duchu kutoka klabu ya Lipuli Fc pamoja na beki wa kati wa Coastal Union Ibrahim Ame
Kuna nyota kadhaa wa kigeni wanaohusishwa na mabingwa hao wa nchi akiwemo beki wa kimataifa wa Burundi na Klabu ya Chippa United ya Afrika kusini Frederic Nsubaiyumva