Okwi anawapenda mashabiki wa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Jan 2018
Okwi anawapenda mashabiki wa Simba
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, amesema mabao mawili aliyoyafunga katika mchezo wa juzi dhidi ya Majimaji ni maalum kwa mashabiki wa timu ya Wekundu wa Msimbazi.

Magoli hayo mawili aliyofunga katika ushindi wa mabao 4-0 yamemfanya sasa mshambuliaji huyo raia wa Uganda kufikisha mabao 12 kwenye ligi msimu huu na kuongoza kwa idadi kubwa ya mabao.

"Nawashukuru mashabiki wanaoendelea kutusapoti na kututia moyo katika kila mchezo, mabao haya niliyoyafunga leo ni kwa ajili yao," alisema Okwi.

"Tutaendelea kupambana kuhakikisha tunafikia malengo yetu ya kutwaa ubingwa msimu huu, na hilo linawezekana," aliongeza kusema Okwi.

Okwi amedhihirisha kuwa hatari zaidi pindi Simba inapocheza jijini Dar es Salaam, kwani mpaka sasa hajaifungia timu hiyo bao lolote nje ya viwanja vya Dar es Salaam.

Hiyo inamaanisha mabao yote 12 ameyafunga kwenye viwanja vya Uhuru na Uwanja wa Taifa.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’