Msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom unatarajiwa kufunguliwa August 29 kwa mchezo utakaozikutanisha Simba na Namungo Fc
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha
Rais wa Shirikisho la Mpira wa MIguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema kwa mujibu wa kanuni, Simba mabingwa wa ligi kuu pamoja na kombe la FA watakutana tena na Namungo Fc iliyofanikiwa kucheza fainali ya michuano hiyo na kufungwa mabao 2-1 na Simba
Kama kanuni za zamani zingetumika, mchezo huo ungezikutanisha Simba na Yanga
SImba imetwaa Ngao ya Jamii kwa misimu mitatu mfululizo, pengine watakuwa na nafasi ya kuchukua Ngao hiyo kwa msimu wa nne
ADVERTISE HERE