Mabingwa nchi Simba wamewasili salama kutoka Mbeya walikounganisha ndege ya jijini Dar es salaam wakitokea mkoani Rukwa ambako jana walitwaa ubingwa wa FA kwa kuichapa Namungo Fc mabao 2-1
Mashabiki wa Wekundu hao wa Msimbazi, wamejitokeza kwa wingi uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuwalaki machampioni hao ambao msimu huu umekuwa wa mafanikio kwao wakishinda mataji matatu 'treble'
Msafara wa wachezaji wa Simba utabebwa na gari maalum kuelekea Makao Makuu ya klabu hiyo, Msimbazi jijini Dar es salaam



ADVERTISE HERE