Djuma ataja mechi za ubingwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Jan 2018
Djuma ataja mechi za ubingwa Simba
Baada ya duru la kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara kumalizika na Simba kufanikiwa kumaliza ikiwa kileleni, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Mrundi Masoud Djuma, amesema bado hawajamaliza kazi ambayo wamepanga kuifanya msimu huu huku akitaja mechi tatu za kuwapa ubingwa.


Simba inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 35 ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 30 wakati mabingwa watetezi Yanga wako katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 28 huku Singida United wenye alama 27 wakiwa nafasi ya nne.

Djuma amebainisha kuwa kama Simba itapata ushindi katika mechi dhidi ya Yanga, Azam FC na Singida United, watakuwa wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kunyakua ubingwa wa msimu huu.

Djuma alisema kwa sasa hakuna timu yenye uhakika wa kuchukua ubingwa huo, lakini kumaliza wakiwa wanaongoza msimamo kwa tofauti ya pointi tano kutoka klabu inayowafuatia ni jambo jema na litawafanya kupambana kuhakikisha wanaendelea kuwakimbia wapinzani wao.

"Kikubwa tunamshukuru Mungu tumemaliza mzunguko wa kwanza tunaongoza, lakini katika nafasi ya mbio za ubingwa naweza kusema tuna asilimia 55 mpaka pale tutakapocheza na wapinzani wetu, na tutaiona mapema kwa sababu mechi mbili kati ya Azam na Yanga tutacheza nao mapema na hapo tutaona mwelekezo," alisema Djuma.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’