Msimu huu Simba imefanikiwa kutawala soka la Tanzania katika kila nyanja baada ya timu ya Simba Queens nayo kukaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake
Wakiwa na alama 50 baada ya kushuka dimbani mara 19, wababe hao wa soka la Wanawake wanahitaji kushinda mchezo mmoja tu kati ya michezo mitatu iliyopita
Hakuna shaka wanakwenda kumaliza utawala wa JKT Queens kwenye soka la Wanawake
Haya yatakuwa mafanikio makubwa kwa Simba Queens katika msimu wake wa tatu tangu timu hiyo ilipoundwa
Simba Queens inanolewa na mshambuliaji wa zamani wa Simba Mussa Hassan Mgosi

ADVERTISE HERE