Mabingwaaa tena, tena na tenaaaa, FT Namungo 1-2 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Aug 2020
Mabingwaaa tena, tena na tenaaaa, FT Namungo 1-2 Simba

Mabingwa wa nchi Simba wamekamilisha msimu vile walivyotaka baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kuichapa Namungo Fc mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Nelson Mandela huko Sumbawanga

Ilikuwa siku nyingine nzuri kwa Mmakonde Luis Miquissone akifunga bao moja na kutengeneza bao la pili lililofungwa na nahodha John Bocco

Miquissone aliitanguliza Simba kwa bao safi kwenye dakika ya 30 akimalizia kwa guu lake la kulia mpira mpira uliokuwa ukizagaa langoni kwa Namungo

Katika dakika ya 38, Miquissone akamsetia Bocco kuweka kambani bao la pili lililowapa Simba uongozi mpaka wakati wa mapumziko

Pamoja na changamoto ya uwanja, Simba iliweza kumudu kucheza kandanda safi kwa nyakati tofauti, ikiwatumia Kapombe na Tshabalala kumwaga maji langoni kwa Namungo Fc

Bao la kufutia machozi kwa upande wa Namungo lilifungwa na Edward Charles Manyama

Simba imeweka kibindoni taji la tatu msimu huu ikiwa pia imetwaa Ngao ya Jamii na Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa tatu mfululizo

Hii ndio maana halisi ya kuwa mabingwa wa nchi

Hongera Wekundu wa Msimbazi, Hongera Machampioni wa Taifa...!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
19h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’