Mlinda lango namba mbili wa Simba Beno Kakolanya, anatajwa kuwa mbioni kujiunga na Azam Fc, imefahamika
Mkataba wa Beno na Simba unamalizika mwezi huu huku kukiwa hakuna mazungumzo ya mkataba mpya
Juzi Azam Fc ilitangaza kuachana na mlinda lango wake Mghana Razak Abarola ambaye mkataba wake umemalizika na wakati huohuo wakitangaza kuwa nafasi yake itachukuliwa na kipa mzawa
Beno ameshindwa kujihakikishia nafasi mbele Aishi Manula, akipoteza nafasi zaidi baada ya mapumziko ya corona mabosi wake wa benchi la ufundi wakimtaka apunguze uzito
ADVERTISE HERE