Simba yapania kutwaa taji la tatu msimu huu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Aug 2020
Simba yapania kutwaa taji la tatu msimu huu

Mkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck amesema vijana wake wako tayari kuelekea mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Nelson Mandela huko Sumbawanga

Akizungumza na wanahabari baada ya kikao cha mwisho kuelekea mchezo huo, Sven amesema walichofuata Rukwa ni kombe hivyo atatumia silaha zake kamili kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kuongeza taji la tatu msimu huu

"Tumekuja hapa kucheza fainali na kushinda ubingwa. Ni mchezo ambao tunahitaji kushinda hivyo tutatumia wachezaji wetu wote bora ili kuhakikisha tunashinda. Wachezaji wote wapo tayari," alisema Sven

Naye nahodha wa mabingwa hao wa nchi John Bocco amesema pamoja na kuwa wanakutana na moja ya timu bora sana msimu huu, maandalizi waliyofanya yanawapa matumaini makubwa ya kushinda

"Tunaamini tunakutana na mpinzani mzuri, anatujua na sisi tunamjua lakini tunaamini maandalizi yetu na kwa kumtanguliza Mungu tunaamini kesho tunaenda kupambana na kushinda ubingwa wa FA"

"Tunachoangalia sana kesho ni kuandika historia kuchukua makombe matatu msimu huu (Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na kombe la FA). Ni moja ya malengo tangu tunaanza msimu na hiyo ni kama hamasa kwetu ya kutafuta ushindi hapo kesho," alisema Bocco

Mchezo huo utapigwa Jumapili kuanzia saa tisa kamili Alasiri

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’