Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa ameondoka jijini Dar es salaam mapema leo kuelekea Sumbawanga kushuhudia mchezo wa fainali ya kombe la FA (ASFC) kati ya mabingwa wa nchi Simba dhidi ya Namungo Fc
Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa Rukwa, utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Nelson Mandela
Mazingisa ameongozana na Afisa Habari, Msemaji na Mhamasishaji wa 'Machampioni' wa nchi, Haji Manara
Simba imepania kusepa na taji la FA, ili kumaliza msimu na mataji matatu baada ya kuwa tayari wamechukua Ngao ya Jamii na ubingwa wa Ligi Kuu
ADVERTISE HERE