Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom imekamilisha orodha ya awali ya wachezaji 30 wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa
VPL msimu wa 2019/2020 ambao baadaye watapunguzwa na kubaki 10 kisha watatu watakaoingia fainali ili kumpata mshindi.
Wachezaji hao 30 na majina ya timu zao katika mabano ni Nico Wadada, Idd Nado na Obrey Chirwa (Azam FC), Abdulmajid
Mangalo, Daniel Mgore (Biashara United FC), Ayoub Lyanga na Bakari Mwamnyeto (Coastal Union FC), David Luhende, Yusuph Mhilu na Awesu Awesu (Kagera Sugar FC) na Waziri Junior (MbaoFC).
Wengine ni Lucas Kikoti, Bigirimana Blaise na Reliants Lusajo (Namungo FC)
Pia wamo Shomari Kapombe, Meddie Kagere, Aishi Manula, Clatous Chama, Francis Kahata, John Bocco, Jonas Mkude na Luis Miquissone (Simba SC).
Orodha hiyo pia imewajumuisha Mapinduzi Balama, Feisal Salum, Deus Kaseke, David Molinga na Juma Abdul (Young Africans SC), Martin Kigi (Alliance
FC), Daruweshi Saliboko (Lipuli FC), Marcel Kaheza (Polisi Tanzania)
Tuzo ni tarehe 7.8.2020 Mlimani City