Hapa ndipo mahali ambapo mchezo wa fainali kombe la Shirikisho kati ya Namungo Fc dhidi ya Simba utapigwa siku ya keshokutwa Jumapili, August 02
Ni katika uwanja wa Nelson Mandela ambao uko ndani ya Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa
Juhudi kubwa zimefanyika kuweka mazingira ya uwanjani kuwa salama kwa mchezo huo kupigwa kwani ni kwa miaka kadhaa uwanja huo umekosa shamrashamra za kabumbu
Leo maafisa wa TFF walikamilsha maandalizi ya mwisho ikiwa ni pamoja na kuweka milingoti ya magoli
Simba na Namungo Fc, zitaruhusiwa kujifua katika uwanja huo kabla ya mtanange wa fainali hapo Jumapili




ADVERTISE HERE