Vipi huyu mwamba arudi?

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Jul 2020
Vipi huyu mwamba arudi?

Habari za chinichini ni kuwa mabosi wa Simba wanaangalia uwezekano wa kumrejesha mshambuliaji wao Mganda Emmanuel Okwi ambaye kwa sasa anacheza kule Misri klabu ya Ittihad

Katika jitihada za kuboresha kikosi kuelekea michuano ya ligi ya mabingwa, Okwi anaangaliwa kama mchezaji anayeweza kuwa na mchango mkubwa kwenye michuano hiyo

Mwaka juzi akishirikiana wenzake Meddie Kagere na nahodha John Bocco, walifanya mambo makubwa wakiipeleka Simba hatua ya robo fainali ya michuano hiyo

Kama Mganda huyo bado yuko kwenye ubora wake, akirejeshwa atazidi kuing'arisha safu ya ushambuliaji ya Simba ambayo mwanzoni mwa mwaka huu imemuongeza Mmakonde hatari Luis Miquissone

Uzuri wa Okwi ni mchezaji mwenye mapenzi makubwa na Simba, ingawa wakati mwingine hulazimika kufanya maamuzi kwa kufuata maslahi

Kwa Simba haijalishi Okwi ameondoka na kurudi mara ngapi, kwani mchezaji huyo ametimiza wajibu wake ipasavyo mara zote anapokuwa Simba

Ni mchezaji ambaye hupata mafanikio zaidi anapokuwa Simba na mambo humuendea mrama kila anapokuwa nje ya Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’