Mwishoni wa wiki hii siku ya Jumapili, utapigwa mtanange wa fainali ya michuano ya kombe la FA (ASFC) kati ya mabingwa wa nchi Simba dhidi ya Namungo Fc katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Nelson Mandela, mkoani Rukwa, Sumbawanga
Kwa muda mrefu, mkoa wa Rukwa haukushuhudia mechi hizi kubwa kwa kuwa hawana timu inayoshiriki ligi kuu wala ligi daraja la kwanza
Hivyo TFF kuwapelekea mtanange huu ni jambo lililowafurahisha wakazi wa mkoa huo na maeneo ya jirani
Lakini pia TFF walilazimika kuufanyia ukarabati mkubwa uwanja wa Nelson Mandela ili uweze kuwa na hadhi ya kutumika katika mchezo huo




Kwa kiasi kikubwa maandalizi ya uwanja yamekamilika, tayari kwa mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu mkoani Rukwa
ADVERTISE HERE