Msimu wa ligi kuu bara 2019/20 umeshafika tamati na Simba wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.
Ubingwa wa Simba unatoka na vitu vingi ukiachilia mbali magoli 22 ya Meddie Kagere, kuna kazi kubwa imefanywa na kipa namba moja wa Simba Aishi Manula ambaye ana misimu mitatu tu ndani ya Simba.
Msimu huu Manula amefungwa magoli 11 tu huku ikiwa ni muendelezo wa alichokifanya misimu miwili iliyopita, msimu wa 2018/19 alifungwa magoli 13, huku msimu wake wa kwanza akiwa akifungwa magoli 12 tu
Hii ni rekodi ya kipekee maana yake wastani ndani ya misimu mitatu aliyokaa Simba Manula amecheza michezo 18 kati ya 30 bila kufungwa
Hongera kipa namba moja wa nchi, Aishi Manula..!
ADVERTISE HERE