Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kimeanza maandalizi ya kuelekea mchezo wa fainali michuano ya kombe la FA dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa August 02 mkoani Rukwa
Simba iliwasili Mbeya jana ikitokea mkoani Kilimanjaro ambako ilikamilisha msimu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania
Mabingwa hao wa nchi, wameanza maandalizi yao leo asubuhi kabla ya safari ya Rukwa
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema watakuwepo mkoani Mbeya kwa siku tatu kujiandaa na mchezo huo
"Tumewasili salama hapa Mbeya, wachezaji wote wako katika hali nzuri na leo asubuhi tumeanza mazoezi, tukitarajia kuweka kambi ya siku tatu hapa," alisema Rweyemamu
Aidha wakati Simba ikijichimbia Mbeya, wapinzani wao Namungo Fc nao wamewasili mkoani humo wakijifua