Mo apendekeza uwanja wa Taifa uitwe uwanja wa Mkapa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Jul 2020
Mo apendekeza uwanja wa Taifa uitwe uwanja wa Mkapa

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Mohammed Dewji 'MO' amewataka wadau wa soka na Watanzania wamuunge mkono katika kampeni aliyoianzisha kisha kuwasilisha mapendekezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli akubali maombi ya kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa Uwanja wa Benjamin William Mkapa

Mzee Mkapa aliyefariki dunia juzi, ndiye aliyefanikisha ujenzi wa Uwanja huo wakati wa uongozi wake wa Awamu ya Tatu

"Leo nimeamua kuanzisha petition (maombi) kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa: Uwanja wa Benjamin William Mkapa," aliandika Mo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

"Ujenzi wa Uwanja wa Taifa wa jijini Dar es Salaam ulianzishwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa. Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ni miongoni mwa viwanja bora katika bara la Afrika kwa sasa.

"Uwanja huo kwa namna mmoja au nyingine umesaidia kuendeleza mpira wa miguu na michezo mingine nchini Tanzania. Uzuri na ukubwa wa soka letu umedhihirishwa kwa sababu ya uwanja wetu huo ambao unashika nafasi ya 11 kwa ukubwa Afrika.

"Uwanja huo wa kisasa umeongeza uzalendo mkubwa kwa kuwezesha maelfu ya mashabiki kuwa sehemu ya michezo yote mikubwa, pia umeongezea mapato kwa klabu zote na kutuletea heshima kubwa nchini na mifano ipo dhahiri.

"Kutokana na uzuri wa uwanja huo, klabu zote za nje ambao huja kucheza katika uwanja huo zimekuwa zikitoa sifa mbalimbali. Timu za mataifa makubwa kama Brazil zimecheza kwenye uwanja huo na kumwaga sifa mbalimbali.

"Nje ya michezo, mashindano ya usomaji wa Quran yaliona mkusanyiko mkubwa zaidi kwenye mashindano makubwa ya kusoma Quran barani Afrika, hii nayo ilikuwa ni rekodi nzuri kwetu Watanzania.

"Tumeshuhudia matamasha mbalimbali makubwa kama matamasha ya Pasaka na Krsimasi yakifanyika hapo na lengo la yote hayo ni kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

"Itakuwa ni heshima kubwa kama uwanja wetu pendwa utaitwa jina la Uwanja wa Benjamin William Mkapa. Tunamuomba Rais John Pombe Magufuli aridhie kubadili jina la uwanja huo kwa heshima ya Hayati Mkapa ili tuendelee kumkumbuka kwa mchango wake mkubwa na hasa kwa vizazi vijavyo.

"Tunawaomba Watanzania wote bila kujali ushabiki wa klabu muunge mkono kwa kuweka sahihi ili tumuombe Mhe Rais kubadilisha jina la uwanja huo uitwe Benjamin William Mkapa Stadium au Uwanja wa Benjamin William Mkapa"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’