Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba jioni ya leo kitakuwa uwanja wa Ushirika mjini Moshi kuumana na Polisi Tanzania katika mchezo wa mwisho wa kukamilisha msimu wa 2019-20
Ni mchezo usiokuwa na presha kwa timu zote, Simba wakiwa tayari ni mabingwa kwa msimu wa tatu mfululizo wakati Polisi Tanzania wamejihakikishia kubaki Ligi Kuu
Lakini ni mchezo ambao Simba itautumia kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Namungo Fc
Upo uwezekano mkubwa kocha Sven Vandenbroeck atawapumzisha nyota wake muhimu ili kuwaepusha na majeraha kabla ya mechi ya fainali, FA
Simba ilikamilisha maandalizi yake ya mwisho jana katika uwanja wa Ushirika tayari kwa mchezo huo
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni sambamba na michezo mingine tisa ya kukamilisha msimu wa ligi kuu
Vita kubwa iko katika timu zinazojinusuru kuteremka daraja, vilabu saba vikiwa hatarini
Vilabu hivyo ni Ndanda, Alliance Fc, Mwadui Fc, Mtibwa Sugar, Mbao Fc, Lipuli Fc na Mbeya City
Timu tatu zitaungana na Singida United kuteremka daraja wakati timu mbili zitakwenda kucheza play-off