Rais Mstaafu Awamu ya tatu Mh Benjamini Mkapa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Hospitalini jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amethibitisha kutokea kwa msiba huo ambapo ametangaza siku saba za maombolezo
Huu ni msiba mkubwa kwa Tanzania kwani kama nchi bado tulihitaji mchango na uzoefu wa Mzee Mkapa
Mzee Mkapa ataendelea kubaki katika kumbukumbu za Watanzania wote wakiwemo wadau wa soka ambao watamkumbuka kwa kujenga uwanja mkubwa wa Taifa ambao unachukua mashabiki elfu 60
Kifo chake kimetokea wakati nchi ikielekea kufanya uchaguzi mkuu Oktoba 28 2020

Mwenye ez Mungu ailaze roho yake mahali pema, peponi AMEN..
ADVERTISE HERE