Jana Simba imedhihirisha kuwa timu zinazoitafuta ili kuishika katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara zina kazi baada ya kuzidi kujiimarisha kileleni mwa ligi hiyo kwa pointi na utajiri wa mabao.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Taifa jana, Simba ilihitimisha mzunguko wa kwanza kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majmaji ya Songea, hivyo kufikisha jumla ya pointi 35 na mabao 35 wakati nyavu zake zikitishwa mara sita tu.
Nahodha John Bocco 'Adebayor' na straika Mganda Emmanuel Okwi ndiyo walioibuka mashujaa katika mechi hiyo kwa kufunga mabao mawili kila mmoja katika mechi hiyo ambayo Simba ilitawala mwanzo mwisho.
Kwa mabao hayo, Okwi anaendelea kuwa kileleni mwa wafungaji bora akiwa amecheka na nyavu mara 12 katika mzunguko huu wa kwanza wakati Simba, ikiwa kileleni kwa pointi tano zaidi dhidi ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili na saba dhidi ya Yanga iliyopo nafasi ya tatu.
Matokeo hayo ni mwanzo mzuri kwa kocha Mfaransa Pierre Lechantre, ambaye jana alikiongoza kikosi hicho kwa mara ya kwanza tangu akabidhiwe rasmi mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog aliyetimuliwa.

ADVERTISE HERE