Nyota hawa wanaweza kutemwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Jul 2020
Nyota hawa wanaweza kutemwa Simba

Mabingwa wa nchi Simba kwa sasa wanakamilisha ratiba tu kwenye ligi wakisubiri mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa kule Sumbawanga August 02 2020

Inaelezwa tayari hesabu za kuelekea msimu mpya zimeanza na pengine baada ya mchezo dhidi ya Namungo, majina ya wachezaji watakaotemwa yatawekwa hadharani ili kuwapa muda wa kusaka maisha mahali pengine

Umekuwa ni utaratibu wa Simba kuachana na wachezaji kistaarabu na ndio maana wengine huweza kurejea pale viwango vyao vinapoimarika

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa ameweka bayana kuwa hawatafanya usajili mkubwa sana kama ilivyokuwa msimu uliopita kwani timu haina mapungufu makubwa

Kwa maana hiyo hata idadi ya wachezaji ambao wataachwa haiwezi kuwa kubwa

Idadi ya nyota wapya haitazidi watano huku idadi kama hiyo itakuwa kwa wachezaji watakaoonyeshwa mlango wa kutokea

Miongoni mwao inaelezwa ni kiungo Msudan Sharaff Elden Shiboub ambaye ameshindwa kupenya kwenye kikosi cha kocha Sven Vandenbroeck

Shiboub hajajumuishwa katika safari ya mkoani Tanga na inaelezwa pengine yuko mbioni kuondoka nchini baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kukwama

Tairone Santos, beki huyu kutoka Brazil naye safari yake imewadia baada ya kuwatumikia mabingwa hao wa nchi kwa msimu mmoja tu

Wakati yeye akiondoka, mwenzie Gerson Fraga amejihakikishia kuendelea kubaki Msimbazi, akisubiriwa kusaini mkataba mpya

Kwa upande wa wachezaji wazawa ambao wako kwenye hatihati ya kuachwa ni mlinzi wa kulia Haruna Shamte na beki wa kati Yusufu Mlipili

Kuimarika kwa kiwango cha Kennedy Juma, kumemuweka matatani Mlipili kwani Simba inatarajiwa kusajili beki mwingine wa kati atakayeshirikiana na hawa waliopo

Dirisha la usajili litafunguliwa rasmi wiki ijayo, August 01

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’