Mabingwa wa nchi Simba jioni ya leo watashuka kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kumenyana na Coastal Union katika moja ya michezo miwili ya kukamilisha msimu
Huu ni mchezo wa heshima tu kwa Simba, kocha Sven Vandenbroeck huenda akawapa mapumziko baadhi ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza wasubiri mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Namungo Fc
Simba iliwasili jijini Tanga juzi jioni na jana ikapata nafasi ya kufanya maandalizi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Mkwakwani
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Simba mapema leo, wachezaji Gerson Fraga na Luis Miquissone watakosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Aidha Ibrahim Ajib, Sharaf Shiboub, Rashid Juma, Haruna Shamte, Shiza Kichuya, Cyprian Kipenye na Tairone Do Santos wao hawakusafiri na kikosi wamebaki jijini Dar es Salaam.