Kocha Mkuu wa mabingwa wa nchi, Simba Sven Vandenbroeck amepania kushinda michezo miwili iliyosalia, ukiwemo dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, ili kukamilisha ratiba ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2019/2020 na kufikisha alama 90
Simba ambao hadi sasa wamekwishatangazwa mabingwa wa ligi na kutete kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kufikisha pointi 84 ambazo haziwezi kufikiwa na timu zingine kati ya 20 zinazoshiriki ligi hiyo inayoelekea ukingoni
Akizungumza jana kabla ya safari ya mkoani Tanga, Sven alisema pamoja na kuwa hawana presha na mechi hizo zilizobaki, wanahitaji kufanya vizuri kulinda heshima yao
"Bado tunajukumu la kupata ushindi kwenye mechi zote mbili zilizosalia tuendelea kuwapa burudani mashabiki wetu ambao muda wote wamekuwa wakituunga mkono," alisema Sven
Kama Simba itashinda mechi hizo (dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania) itafikisha alama 90
Aidha michezo hiyo pia itakuwa sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Simba kuelekea mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa August 02 mkoani Rukwa