Simba Queens imeendelea kulikaribia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu soka la Wanawake Tanzania Bara baada ya kuifunga Kigoma Sisters kwa mabao 3-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma juzi.
Ushindi huo uliifanya Simba Queensime ifikishe pointi 44 baada ya kucheza michezo 17 ikifuatiwa na JKT Queens ambayo ina pointi 39 baada juzi kuifunga Panama katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo mabao ya Simba Queens mawili yalifungwa na Oppah Clement na Mwanahamisi Omar na lile la Kigoma Sisterz lilifungwa na Aisha Hamza na Kigoma kuendelea kubaki na pointi zake 23.
Huu utakuwa msimu mzuri kwa timu zote za klabu ya Simba, kwani timu ya Wanaume tayari imeshatwaa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo