Sven kuongezewa mkataba Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Jul 2020
Sven kuongezewa mkataba Simba

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ana nafasi kubwa ya kuongezewa mkataba na mabingwa hao wa nchi licha ya tetesi za ujio wa kocha wa AS Vita Florente Ibenge

Pamoja na kuanza maisha yake katika klabu ya Simba kwa kusuasua, kwa kiasi kikubwa, Sven anaonekana kuirejesha timu katika makali yake ya msimu mmoja nyuma ikicheza kandanda safi na sasa ikifunga mabao mengi

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye hakutaka jina lake liwekwe hadharani, amesema kuwa Sven ataendelea kubaki Msimbazi kwani litakuwa jambo la kushangaza kumuondoa kocha huo kutokana na mafanikio aliyopata

"Tulianza msimu vibaya lakini furaha yetu Sven ameirejesha kwa kutuwezesha kutwaa ubingwa wa ligi kuu mapema pamoja na kutinga fainali ya michuano ya kombe la FA. Lakini pia timu yetu inaonekana kuimarika, vijana wanacheza kandanda safi. Nakuhakikishia, tutaendelea kuwa na Sven kwa msimu ujao pia wa 2020-2021," alisema

Hivi karibuni Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa alisema baada ya kutwaa ubingwa na kutinga fainali ya FA, sasa wanaelekeza nguvu kwenye maboresho ya kikosi kuelekea msimu ujao wakijipanga kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

Sven tayari amewasilisha mapendekezo ya maboresho anayotaka, ikielezwa Simba huenda ikaongeza nyota wanne tu

Alipojiunga na Simba mwezi Disemba 2019, Sven alipewa mkataba wa miezi sita ambao unamalizika baada ya msimu kufika tamati wiki ijayo

Lakini ni wazi Mbelgiji huyo atapewa mkataba mpya

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
20m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
21h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’