FT : Simba 4-0 Majimaji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Jan 2018
FT : Simba 4-0 Majimaji
Simba imemaliza mzunguuko wa kwanza ligi kuu ya Vodacom kwa staili ya aina yake baada ya kuifumua Majimaji mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa kocha mpya Pierre Lechantre ambaye hata hivyo hakukaa kwenye benchi la Simba kutokana na kutokuwa na kibali.

Simba iliuanza mchezo huo polepole hata hivyo ilichangamka baadae na kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Majimaji.

Nahodha John Bocco 'Adebayor' ndiye aliyeanza kuifungia Simba kwenye dakika ya 17 kisha dakika ya 27 akafunga la pili akiitendea haki mipira ya krosi ya Said Juma 'Ndemla' na kona ya Shiza Kichuya.



Simba iliyokuwa 'on-fire' iliendelea kulisakama lango la Majimaji na alikuwa kinara wa mabao, Emanuel Okwi aliyefunga mabao mengine mawili.

Kwenye dakika ya 51 Okwi alifunga bao la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi ya Shiza Kichuya kabla hajapachika la nne kwenye dakika ya 68 kwa kumchambua mlinda lango baada ya kupokea pasi ya Bocco.

Katika mchezo huo kocha wa Simba Pierre Lechantre alibadili mfumo wa kikosi chake kutoka 3-5-2 na kutumia 4-1-3-2.



Matokeo hayo yameifanya Simba imalize mzunguuko wa kwanza ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo.

Imejikusanyia alama 35, alama tano mbele ya Azam FC iliyo nafasi ya pili.

Imefunga mabao 35 na kufungwa mabao sita pekee. Imefunga mabao 15 zaidi ya Yanga iliyofunga mabao 20 pekee msimu huu.

Kwenye mzunguuko wa kwanza imejivunia utajiri mkubwa wa mabao (GD) +29 wakati timu inayoifuatia ni Yanga yenye GD +12

Emanuel Okwi anaongoza orodha ya wapachika mabao akiwa amefunga mabao 12 akifuatiwa na John Bocco, Obrey Chirwa, Mohammed Rashid na Habibu Kiyombo ambao wote wana mabao saba kila mmoja.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’