Mabingwa wa nchi Simba wamewaaga kibabe wakazi wa jijini Dar es salaam na maeneo ya jirani baada ya kuifumua Alliance Fc mabao 5-1 katika mchezo wa mwisho msimu huu kwa Simba kutumia uwanja wake wa nyumbani
Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Mbao Fc, leo kocha Sven Vandenbroeck hakutaka utani baada ya kushusha kikosi chake cha kwanza, na matkeo yake Alliance wamekutana na kipigo cha mbwa mwizi
Meddie Kagere 'Mk 14' leo ameingia kambani mara mbili akifikisha mabao 22 na kuzidi kujikita kileleni katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu
Ni wazi Kagere ataondoka na kiatu hicho kwa msimu wa pili mfululizo anachotafuta sasa ni kuvunja rekodi yake ya mabao 23 aliyoweka msimu uliopita
Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Luis Miquissone, Saidi Ndemla na Deo Kanda
Simba sasa itaelekea mkoani Tanga kuikabili Coastal Union kisha kuelekea Moshi kukamilisha msimu kwa kuivaa Polisi Tanzania

