Kesho Jumapili mabingwa wa nchi Simba watacheza mchezo wao wa mwisho jijini Dar es salaam msimu huu kwa kuikabili Alliance Fc katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Taifa
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kupata burudani kutoka kwa timu yao
Amesema kwa kuwa ni mchezo wa mwisho kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na maeneo ya jirani, watarajie kukiona kikosi kamili ambacho kitawajumuisha nyota walioiadhibu Yanga kipigo cha mabao 4-1 wiki iliyopita
Simba ilipoteza mchezo wa ligi uliopita kwa kufungwa mabao 3-2 na Mbao Fc katika mchezo ambao kocha Sven Vandenbroeck alibadili kikosi chote cha kwanza
ADVERTISE HERE