Beki kiraka Erasto Nyoni amesema hawakutarajia kupoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc na sasa wamesahau matokeo hayo wakijiandaa na mchezo unaofuata
Jana Simba ilifungwa mabao 3-2 na Mbao Fc waliopambana kwelikweli wakihitaji kujinusuru na janga la kuteremka daraja
Tangu ichukuliwe na kocha Fred Felix Minziro, Mbao Fc imeshinda mechi tano mfululizo
"Ulikuwa mchezo wenye ushindani, tulicheza vizuri kwa muda mwingi, lakini hatukutumia nafasi nyingi tulizotengeneza, wenzetu wakatumia makosa yetu kutuadhibu"
"Haukuwa mchezo mwepesi kama wengi wanavyodhani kwani kwenye ligi hakuna timu ndogo, kila timu inapambana kufikia malengo yake. Tumesahau matokeo hayo tunajiandaa na mchezo unaofuata," alisema Nyoni ambaye alikuwa nahodha wa kikosi cha Simba siku ya jana
cutSimba ambayo tayari ni mabingwa wa ligi kuu, itashindwa kufikia rekodi yake ya pointi waliyoweka msimu uliopita sasa wakiwa na uwezo wa kufikisha alama 90 kama watashinda mechi tatu zilizobaki
Msimu uliopita Simba ilitwaa ubingwa ikiwa na alama 92
Katika michezo minne ya ligi, mabingwa hao wamepoteza mchezo mmoja na kutoka sare michezo mitatu
Haya ni matokeo ambayo kwa mara ya kwanza Simba wameyapata mfululizo msimu huu
Hata hivyo hayana maana yoyote kwa kuwa tayari taji la tatu mfululizo limetulia pale Msimbazi hivyo mechi zilizobaki ni za kukamilisha ratiba tu