Mbao Fc imefanikiwa kuondoka na alama zote tatu mbele ya mabingwa wa nchi Simba kufuatia ushindi wa mabao 3-2 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck alifanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake kilichoshuka dimbani leo akiwaacha nje wachezaji wote walioifumua Yanga mabao 4-1 kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la FA mapema wiki hii
Mbao Fc inayopambana kujinusuru na kuteremka daraja, ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya tano tu kupitia kwa Rajabu Rashid
Meddie Kagere akairudisha Simba mchezoni kwenye dakika ya 35 kwa mkwaju wa penati baada ya Gadiel Michael kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari
cutWaziri Junior akaiongezea Mbao Fc bao la pili kabla Miraji Athumani hajaisawazishia Simba
Bao la ushindi kwa Mbao Fc lilifungwa na Jordan John
Simba iliingia kwenye mchezo huo ikiwa haina cha kupoteza, pengine ndio sababu Sven alipata uhuru wa kubadili kikosi chote
Mabingwa hao wa nchi wanatarajiwa kucheza na Alliance Fc siku ya Jumapili kabla ya kuelekea mkoani Tanga kuifuata Coastal Union na kisha kwenda kumaliza msimu kule Moshi kuikabili Polisi Tanzania