Beki Shomari Kapombe amemwagia sifa Kocha Msaidizi wa Simba, Masudi Djuma kwa kumrejesha upya uwanjani akiwa na moto kama zamani licha ya kutoka kwenye majeraha.
Kapombe aliyesajiliwa akitokea Azam, hakuwa amecheza mechi kwa miezi sita tangu alipoumia akiwa na timu ya taifa, lakini Jumatatu iliyopita alishuka dimbani kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar.
“Nashukuru viongozi kwa kunivumilia nilipokuwa majeruhi, lakini Djuma amenifanya nirudi kwa kasi kwani aliniambia nina uwezo na nipo vizuri licha ya kutoka majeruhi. Aliniambia lazima nicheze dhidi ya Kagera na kipindi cha pili alinipa nafasi na kusaidia ushindi kwa timu yangu,†alisema.
Naye Kocha Djuma alimwagia sifa beki huyo kwa kusema: “Kapombe ni mchezaji mzuri anayefiti katika mfumo wangu, kama ataendelea kuimarika zaidi atakuwa mtamu sana,†alisema Djuma.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE