Juzi katika mchezo dhidi ya Yanga, kiungo Clatous Chotta Chama 'CCC' maarufu kama mwamba wa Lusaka, ndiye aliyekuwa mpishi wa mambo akihusika kikamilifu katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Yanga
Pamoja na kufunga bao moja, Chama ndye aliyepika bao la kwanza lililowekwa kimiani na kiungo 'mgumu' raia wa Brazil Gerson Fraga
Unaambiwa juzi maji yalizidi unga eneo la kiungo la Yanga kwani Chama akishirikiana na Jonas Mkude, Gerson Fraga, Luis Miquissone na Francis Kahata waliwapoteza kabisa viungo wa Yanga ambao muda mwingi walikuwa wakiutafuta mpira kwa tochi
Huyu ndiye mwamba wa Lusaka ambaye kwake mpira unatii maelekezo bila 'shuruti'
Chama ndiye kinara wa pasi za mabao kwenye kikosi cha Simba akitoa 'asisti' nane kwenye ligi huku mwenyewe akifunga mabao mawili
Simba iko mbioni kumpa mkataba wa muda mrefu ili kuhakikisha anaendelea kubakia Msimbazi. Bado ana mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa hao wa nchi