Simba haiachi kitu, Mbao Fc wajiandae

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Jul 2020
Simba haiachi kitu, Mbao Fc wajiandae

Pamoja na kuwa tayari wametwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa tatu mfululizo, mabingwa wa nchi Simba wamepania kushinda mechi zote zilizobaki kwenye ligi pamoja na mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa August 02

Simba imebakisha michezo minne ya ligi ambayo ni dhidi ya Mbao Fc na Alliance ambayo itapigwa jijini Dar es salaam na michezo dhidi ya coastal Union (Tanga) na Polisi Tanzania (Moshi) na ule wa FA dhidi ya Namungo ukipigwa Rukwa

Nahodha wa wababe hao wa soka nchini John Bocco amesema hawatakuwa na huruma kwa timu yoyote itakayokuja mbele yao na lengo lao ni kushinda mechi zote

Akizungumza baada ya mazoezi mapema leo, Bocco amesema wameshamaliza shangwe la ushindi dhidi ya Yanga na sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mechi zilizobaki

"Baada ya mchezo wa Yanga tumerejea mazoezini kuweka miili sawa kuelekea mchezo wetu dhidi ya Mbao Fc ambao utapigwa Alhamisi (kesho). Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini wajipange kwani tumepania kushinda kila mchezo unaokuja mbele ili tuvune alama nyingi," alisema Bocco

Wachezaji wote walishiriki mazoezi ya lei asubuhi, ambapo nyota walioiangamiza Yanga juzi walifanya program tofauti ya mazoezi huku wale waliokosa nafasi kwenye mchezo huo wakifanya mazoezi tofauti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
43m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’