Wachezaji wa Simba wamemshukuru na kumpongeza mwekezaji wa klabu hiyo Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, kwa kujitoa kuhakikisha timu hiyo inafanikisha malengo iliyojiwekea
Nahodha wa mabingwa hao wa nchi John Bocco amesema Mo ni kila kitu kwao, amekuwa na mchango mkubwa kwa mafanikio ya klabu
Amesema, wachezaji wanajivunia kucheza katika klabu hiyo chini ya uongozi wake
"Tunajisikia furaha kucheza Simba, tunatambua na kuthamini yale yote anayofanya mwekezaji (Mo) kwa ajili ya klabu. Tunakushukuru sana," alisema Bocco
Pamoja na kuanza msimu kwa kusuasua baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa katika hatua za awali, yalikuwa ni matokeo ya huzuni ambayo yaliwaumiza Wanamsimbazi wote
cutLakini ubingwa wa wapema wa ligi kuu na kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Yanga juzi, kimerejesha furaha ya viongozi, wachezaji, mashabiki na wadau wote wa klabu ya Simba
Aidha mafanikio hayo yameshusha 'neema' kwa wachezaji wakivuna mamilioni ya fedha kutoka kwa wadhamini
Kazi iliyobaki ni kukamilisha 'dabo' kwa kutwaa taji la FA, mchezo wa fainali dhidi ya Namungo Fc ukitarajiwa kupigwa August 02 kwenye uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa