Simba yapania kubaki kileleni hadi ubingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
28 Jan 2018
Simba yapania kubaki kileleni hadi ubingwa
Kikosi cha Simba leo Jumapili, Januari 28 kitashuka kwenye dimba la Uhuru kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Majimaji.

Kuelekea mchezo huo, Afisa Habari wa Simba Haji Manara amsema kukaa juu ya msimamo wa ligi kuna raha yake lakini haitakuwa na maana endapo watapoteza au kutaka sare kwenye mchezo wa leo.

“Wachezaji wetu wameahidi kujituma kuhakikisha tunapata pointi tatu ili kuendelea kukaa juu kwa uhuru zaidi, pale juu pana raha yake najua kwa matokeo yoyote ya mechi yetu na Majimaji tunaendelea kukaa juu, lakini haitakuwa na maana kama unakaa juu huku umefungwa au umetoka draw raha ya kukaa juu uwe umeshinda tena ushindi mzuri.”

Manara amesema majimaji ni timu nzuri wanaiheshimu kwa historia yake kwenye soka la bongo pamoja na rekodi yao nzuri ilipokutana na timu zinazofanya vizuri msimu huu.

“Ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri na rekodi zao ni nzuri kwa timu ambazo zinafanya vizuri msimu huu Yanga, Singida United, Azam na hata Prisons hakuna timu iliyowafunga Majimaji kwa hiyo sisi hatuendi pale tukiwa tunawadharau, tunajua tunahitaji pointi tatu.”

Kuhusu presha ya Azam na Yanga ambazo zipo nyuma yao, Manara amesema, timu hizo haziwashughulishi wanachoangalia ni timu wanayokutananayo.

“Hawa wa nyuma tusishughulike nao sana, sisi tushughulike na na yule tunayecheza nae, tukishinda mechi zetu zote hawa wanyuma vyovyote itakavyokuwa hawatushughulishi. Lazima tuangalie anayekuja kucheza na sisi tusimwangalie Azam Yanga, Singida United hao tayari wapo nyuma yetu kama tutaendelea kushinda mechi zetu hata wafanye nini hawawezi kutufikia.”
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →