Baada ya kutoa dozi 'heavy' kwa watani zao Yanga kwa kuwafumua mabao 4-1, kikosi cha Simba leo kinarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Alhamisi kwenye uwanja wa Taifa
Mchezo huo ni sehemu ya michezo ya kukamilisha ratiba tu kwenye ligi kwani mabingwa hao wa nchi tayari 'wameshasepa' na kombe kwa msimu wa tatu mfululizo
Watakamilisha ratiba ya ligi kuu kwa kuzivaa Alliance Fc, Coastal Union na Polisi Tanzania kisha kujiandaa na mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Namungo Fc
Huu ndio mchezo unaosubiriwa kwa hamu, Simba ikiwa na hesabu ya kuweka kibindoni mataji mawili msimu huu
ADVERTISE HERE