Kagere, Bocco wachezaji bora VPL March, June

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Jul 2020
Kagere, Bocco wachezaji bora VPL March, June

Mshambuliaji wa Simba kinara wa mabao Meddie Kagere ameibuka kuwa mchezaji bora wa mwezi March 2020 ligi kuu ya Vodacom

Kagere anayeongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akiwa na mabao 19, ametwaa tuzo hiyo akifunga mabao manne katika mwezi huo kabla ya ligi kusimama kutokana na Corona

Kagere amekamata tuzo hiyo baada ya kuwashinda Paulo Nonga wa Lipuli na Never Tigere wa Azam FC alioingia nao fainali

Nae kocha wa KMC ya Dar es Salaam, Hererimana Haruna amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020

Hererimana alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake Sven Vandenbroeck wa Simba na Khalid Adam wa Mwadui FC alioingia nao fainali

Kocha wa Alliance ya Mwanza, Kessy Mziray yeye amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020

Mziray alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake Sven Vandenbroeck wa Simba na Luc Eymael wa Young Africans alioingia nao fainali.

Aidha, mshambuliaji wa Simba, nahodha John Bocco amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020

Bocco alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake Atupele Green wa Biashara United na Martin Kiggi wa Alliance FC alioingia nao fainali

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
20h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
2d ago
READ MORE β†’