Baada ya kumaliza kazi iliyokuwa ikisubiriwa na wengi kwa kuifumua Yanga mabao 4-1, kikosi cha Simba ni kama kimebaki na mchezo mmoja tu mkubwa, fainali ya kombe la FA dhidi ya Namungo ambao utapigwa August 02 uwanja wa Nelson Mandela huko Sumbawanga
Ni wazi kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck atatumia mechi za ligi zilizobaki kuwapa nafasi wachezaji wengine waliokosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Hizi zitakuwa mechi kwa baadhi ya wachezaji kulishawishi benchi la ufundi ili waendelee kubaki Msimbazi
Mchezo wa kwanza utachezwa siku ya Alhamisi dhidi ya Mbao Fc, mchezo huo ukipigwa uwanja wa Taifa
Julai 19 watacheza na Alliance Fc hapohapo Taifa kabla ya kusafiri mkoani Tanga kuifuata Coastal Union kwa ajili ya mchezo mwingine utakaopigwa Julai 23
Simba itakamilisha msimu kwa kuumana na Polisi Tanzania kule wilayani Moshi Julai 26