Baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Yanga jana, kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amewapa wachezaji wake mapumziko ya siku mbili
Akizungumza baada ya mchezo jana, Sven alieleza kufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na vijana wake
Simba itarejea mazoezini kesho Jumanne kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mbao Fc ambao utapigwa Alhamisi Julai 16 kwenye uwanja wa Taifa
"Yanga ilicheza vizuri dakika 15 za mwanzo na vile walivyopata bao moja ila muda wote sisi tulikuwa bora"
"Nawapongeza wachezaji kwa kazi nzuri waliyofanya na nimeridhika na kiwango na nimefurahishwa na ushindi
"Tutarudi mazoezini Jumanne kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mabao siku ya Alhamisi," alisema Sven
ADVERTISE HERE