Nahodha wa Simba John Bocco, amesema ushindi mnono waliopata dhidi ya watani zao Yanga umedhihirisha kuwa wao ndio wababe wa soka la hapa Tanzania
Simba jana waliwafumua watani zao Yanga mabao 4-1 katika mchezo walioutawala kwa muda mwingi
"Sisi ndio Simba na sisi ndio mabingwa, pongezi nyingi kwa wachezaji,benchi la ufundi,viongozi wetu pamoja na mashabiki wetu," alisema Bocco
Mabao ya Gerson Fraga, Clatous Chama, Luis Miquissone na Mzamiru Yassin yalitosha kuzima ndoto za Yanga kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao
Ni rasmi, Simba na Namungo ndizo zitakazoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya CAF msimu ujao, Simba ikicheza ligi ya mabingwa na Namungo wakicheza kombe la Shirikisho
Ni ushindi uliorejesha heshima ya Simba mahali pake baada ya kutopata ushindi katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Yanga
Mashabiki wa Simba wametamba kuwa msimu ujao wataendelea kuwatesa watani zao hao
