FT : Simba 4-1 Yanga, kuna swali?

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Jul 2020
FT : Simba 4-1 Yanga, kuna swali?

Leo Rahaaaaaa..! Wamepasuka vibaya sana, ni kipigo cha mabao 4-1 Yanga imechezea kutoka kwa mabingwa wa nchi Simba katika mchezo ambao wamedhihirisha kuwa hakuna kama wao

Ulikuwa mchezo kati ya Wanaume wa Simba na Wavulana wa Yanga kwani, kwa soka lililopigwa uwanja wa taifa leo, halikuwa la kiwango chao

Dakika ya 21 tu kiungo mwenye roho ya paka, Gerson Fraga alifungua mlango wa mabao Yanga kwa kuweka kambani bao maridhawa akipokea pasi ya Mwamba wa Lusaka, Clatous Chotta Chama

Simba ikaenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0

Waliporejea kipindi cha pili ndipo mauaji yalifanyika, Chama, Miquissone na Mzamiru wakiongeza mabao mengine matatu

Hawa Yanga kipigo chao kiliandaliwa mapema sana, leo ilikuwa siku ya kuwakabidhi zawadi yao

Nadhani ni sahihi kwa sasa kusema kwa hapa Tanzania, Simba hawana mshindani kwani soka la wanalocheza hakika sio la nchi hii

Kipigo cha leo kimewabakisha rasmi Yanga nyumbani kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao, hawatapanda ndege

Badala yao ni Namungo Fc ambao wamejihakikishia kushiriki michuano ya CAF bila ya kujali matokeo ya mchezo wa fainali

Hongera Simba, Hongera mabingwa wa nchi hii...!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’