Bahati haitokei mara mbili - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Jul 2020
Bahati haitokei mara mbili - Manara

Afisa Habari na Msemaji wa klabu ya Simba, mabingwa wa nchi hii, Haji Manara amesema Jumapili watawaadhibu Yanga vikali, wasitegemee bahati waliyoipata kwenye mchezo uliopita kuwa itawatokea tena

Msemaji huyo wa 'Machampioni' ambao jana walirejea kutoka kanda ya Kusini na taji la tatu mfululizo, amesema ni wazi Simba ndio klabu bora zaidi nchini ikiziacha timu nyingine mbali sana

Amesema wao kufungwa na Yanga kwenye mchezo uliopita, ilitokana na wapinzani wao kupata bahati ambayo anaamini haiwezi kutokea mara mbili

"Mchezo uliopita sisi tuliwazidi kila kitu. Tulitengeneza nafasi nyingi zaidi yao na tulicheza mpira mwingi zaidi yao, kilichowasaidia ni bahati tu"

"Sasa nawaambia, Jumapili wasitarajie tena bahati ile, tunakwenda kuwapa adhabu ambao hawataisahau. Hatufikirii matokeo mengine zaidi ya ushindi, hawa hawana ubavu wa kutufunga mara mbili," alitamba Manara

"Juzi Mwekezaji wetu (Mo Dewji) alizungumza na wachezaji na hata mimi nilipata nafasi ya kuzungumza nao wakati tunatoka Mtwara jana, morali yao iko juu sana, kila mmoja anafahamu tuna jambo letu Jumapil"

"Hawa wachezaji baada ya mchezo wetu dhidi ya Prisons kocha aliwapa mapumziko ya siku moja wakazione familia zao lakini walikataa, wakisema wanataka kubaki kambini kuendelea kujiandaa na mchezo wa Jumapili. Nadhani utaona ni kwa jinsi gani wameupa uzito mkubwa mchezo huu"

"Hatuna sababu ya kufungwa na Yanga, tumewazidi kila kitu. Umewahi kusikia wachezaji wetu wakilalamika kutolipwa au kucheleweshewa mishahara kama wengine? Tuna viwanja vizuri, tuna kambi nzuri ambayo ndani yake kuna kila kitu. Tumeshinda ubingwa tukiwa na mechi sita mkononi, lakini pia tumefunga mabao mengi mbali sana kuliko timu nyingine. Hii sio timu ya kufungwa na Yanga mara mbili"

Manara amesema wachezaji wa Simba wanaendelea na mazoezi leo wakitarajia kukamilisha maandalizi ya mwisho kesho kabla ya mchezo huo ambao utakuwa wa kisasi kwa mabingwa hao wa nchi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’