Sven akataa shamrashamra za ubingwa, awapania Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Jul 2020
Sven akataa shamrashamra za ubingwa, awapania Yanga

Kulingana na ratiba iliyokuwa imetolewa na uongozi wa Simba jana, baada ya kuwasili jijini Dar es salaam mabingwa hao wa nchi ambao walikabidhiwa 'mwali' wao kule Ruangwa, walitarajiwa kuongoza shamrashamra za ubingwa kwa kupanda gari maalum la wazi

Hata hivyo kocha Mkuu Sven Vandenbroeck, aligomea mpango huo akitaka wachezaji wake waelekee kambini moja kwa moja kupumzika kisha kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumapili

Sven alisema pamoja na kuwa wametwaa ubingwa wa ligi kuu, bado hawajamaliza kazi hivyo kuanza kusheherekea sasa kunaweza kuwaondoa kwenye malengo yao

Mbelgiji huyo alifanikiwa kuwashawishi viongozi wa Simba ambao waliachana na mpango huo na badala yake kuwaruhusu wachezaji wapande katika moja ya mabasi madogo yaliyokuwepo JNIA kwa ajili ya mapokezi kisha kuelekea kambini

Baada ya kukosa ushindi dhidi ya Yanga katika michezo miwili iliyopita, Sven amepania kumaliza mchezo wa Jumapili mapema tu

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
4h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
4h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
7h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’