Uongozi wa klabu ya Simba umewashukuru mashabiki wake kwa kujitokeza kwa wingi kuilaki timu yao ambayo ilitua mapema leo kutoka Mtwara baada ya kukabidhiwa ubingwa wa ligi kuu
Mabingwa hao wa nchi sasa wameelekea kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumapili
"Asanteni sana mashabiki wetu wote mliojitokeza uwanja wa ndege kutupokea mabingwa wa Ligi Kuu 2019/20. Upendo wenu ni wa kipekee sana"
"Baada ya kuwasili kikosi kimeingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumapili Julai 12, 2020 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam," imesema taarifa ya Simba

ADVERTISE HERE